Hii ni maalumu kwa wasaani wa kitanzani ,ni bora kuwa na mawazo kutoka kwa wadau wa mzik na wenye mawazo endelevu kama baadhi ya wasomi,wasomi wengi wanatakiwa wawe na mambo mengi pia wawe na mawzo kama haya
kwanza wasaani ni watu muhimu sana katika jamii yetu,lakini kuttokana na wanavyojiweka ndo tunawashusha ktk jamii yetu.
msaani ni kampuni ambayo ni kampuni endelevu kama akijipanga na kujiwekea malengo,kwanini nasema msanii ni kampuni?
msanii ni kampuni kwa sababu kuu moja tu,msani yeye ndo anatakiwa aajiri watu ila sio yeye aajiriwe,kama tunavyoona wasanii wetu wakiajiriwa na promoters pamoja na ma redio presenters.
msanii makini mwenye kutaka maendeleo anatakiwa aajiri watu ila sio yeye aajiriwe kwa msanii kuajiriwa ni kumnyonya msanii,msani bora anatakiwa anatakiwa aajiri watu wafuatao
msanii anatakiwa aajiri dj wake
msanii anatakiwa aajiri promoter wake
msanii anatakiwa aajiri marketting manager wake
msanii anatakiwa aajiri disigner wake
msanii anatakiwa aajiri mshauri wake
jamani je tanzania kuna msanii mtanzani mwenye vitu hivi,?ni kazi sana lakini mapinduzi ya muziki naamini ipo siku yatakamilika ,,,,,,,,,naamini kama msanii anaetaka kuenderea lazima ajaribu kufuata hivi.
msanii ni kampuni kwasababu anatakiwa awalipe watu wote hao,so lazima watu hao wafanyye kazi nzuri kwa msanii ndo waweze kulipwa na msanii
lakini hata sisi tunatakiwa tuwashauri wanamuzik wetu ili kuleta maendeleo
wasanii wetu wamekosa vitu muhimu sana kama vifuatavyo
ELIMU
hapa ndo tunaongelea kitu kikubwa sana wasanii wetu hawana elimu, wanafanya kazi kwa kubahatisha tu ukiwauliza wanasema ni kpaji,au mziki upo kwenye damu au nimezaliwa nao haya ni majibu ya kitoto sana na hayafai kusikilizwa mbele ya watu.
MTAJI
msanii antakiwa awe na mtaji wa kutosha ili awe bora na aweze kuwalipa watu wake ,wacheza show wake,dj wake nk.
UBUNIFU,
msanii anatakiwa awe mbunifu wa kazi zake ,wengi watanzania wasanii hujtahidi sana kuwa wabunifu lakini kuna wengine sio wabunifu matokeo yake huiga kazi za wengine na hii haipendezi kwa mwanamziki
msanii anatakiwa awe mbunifu kuanzia kwa jina lake mwenyewe,kazi zake,picha zake,blog yake,nk
hii ni kwa wasanii wetu wa kitanzania jamani tuwashauri wasanii wetu