Friday, February 18, 2011

MABOMU TANZANIA

     Nchi ya Tanzania ni miongoni mwa nchi nzuri zenye amani na upendo,tumekuwa tukiishi kwa amani mda wote huo tangu tulipo pata uhuru,
    Amani sasa imetoweka kwani kila kukicha raia wanapoteza maisha kwa uzembe wa serikari yetu,uongozi usiotazama mbele kazi yake kubwa ni kutatua matatizo ndani ya chama chao ila sio kutatua matatizo ya nchi yetu,
     Mnamo mwaka kama mmoja hivi mbagala ililipuka mabomu ktk kambi ya jeshi huko mbagala,serikali ikazungumzia tu bila kufanya utafiti juu ya mabomu mengine ktk kambi nyingine huu ni uzembe mkubwa wa serikali
      Kama serikali yetu ingekuwa inajari wanainchi wake,ingefanya utafiti juu ya kambi nyingine kuhusu kuona kama je kambi nyingine zinamabomu ambayo hayajapitwa na wakati
      Sasa Gogo la mboto,kumelipuka tena hii inaonyesha kuwa tunaongozwa na viongozi wasiojua kuangalia matukio na kuyafanyia kazi,tukio la kwanza la mbagala linge washitua serikali na kufanya utafiti yakinifu juu ya kambi zetu za jeshi,
      Huu ni uzembe ambayo sisi kama wazalendo wa nchi hii hatuwezi kuvumilia kuona nchii yetu ikipunguza wazalishaji mali wengi kwa makosa ya `uzembe wa serikali yetu.tumechoka kupoteza ndugu jamaa na marafiki zetu kwanini serikali isiweke wataalam wa kuchunguza maswala kama hayo,nchi yetu inakambi nyongi sana je tunazitizama je hizo kambi?
    Sasa tujiulize serikali yetu imejipanga vipi kukomesha milipuko hiyo ya mabomu ambayo humaliza wananchi wenzetu?katika hutuba ya rais wetu hakuzungumzia swaala la kutokomeza ulipukaji wa mabomu katika kambi zetu za jeshi,
     Itakuwaje kama baada ya mwaka mmoja sehemu itayofuata itakuwa ni lugalo?makongo? masaki?itakuwaje kwa taifa
    Serikali yapasa kutambua kuwa mambo haya ya mabomu kuna watu wanaweza kuyaweka yakawa ni mambo ya kisiasa kwani hamna mipango ya kuzuia yasitokee tena.

No comments: