Thursday, February 17, 2011

WANAMUZIKI WA BONGO

Hii ni maalumu kwa wasaani wa kitanzani ,ni bora kuwa na mawazo kutoka kwa wadau wa mzik na wenye mawazo endelevu kama baadhi ya wasomi,wasomi wengi wanatakiwa wawe na mambo mengi pia wawe na mawzo kama haya
     kwanza wasaani ni watu muhimu sana katika jamii yetu,lakini kuttokana na wanavyojiweka ndo tunawashusha ktk jamii yetu.
      msaani ni kampuni ambayo ni kampuni endelevu kama akijipanga na kujiwekea malengo,kwanini nasema msanii ni kampuni?
       msanii ni kampuni kwa sababu kuu moja tu,msani yeye ndo anatakiwa aajiri watu ila sio yeye aajiriwe,kama tunavyoona wasanii wetu wakiajiriwa na promoters pamoja na ma redio presenters.
      msanii makini mwenye kutaka maendeleo anatakiwa aajiri watu ila sio yeye aajiriwe kwa msanii kuajiriwa ni kumnyonya msanii,msani bora anatakiwa anatakiwa aajiri watu wafuatao
                         msanii anatakiwa aajiri dj wake
                         msanii anatakiwa  aajiri promoter wake
                         msanii anatakiwa aajiri marketting manager wake
                         msanii anatakiwa aajiri disigner wake
                         msanii anatakiwa aajiri mshauri wake
        jamani je tanzania kuna msanii mtanzani mwenye vitu hivi,?ni kazi sana lakini mapinduzi ya muziki naamini ipo siku yatakamilika ,,,,,,,,,naamini kama msanii anaetaka kuenderea lazima ajaribu kufuata hivi.
         msanii ni kampuni kwasababu anatakiwa awalipe watu wote hao,so lazima watu hao wafanyye kazi nzuri kwa msanii ndo waweze kulipwa na msanii
 lakini hata sisi tunatakiwa tuwashauri wanamuzik wetu ili kuleta maendeleo
        wasanii wetu wamekosa vitu muhimu sana kama vifuatavyo
     ELIMU
hapa ndo tunaongelea kitu kikubwa sana  wasanii wetu hawana elimu, wanafanya kazi kwa kubahatisha tu ukiwauliza wanasema ni kpaji,au mziki upo kwenye damu au nimezaliwa nao haya ni majibu ya kitoto  sana na hayafai kusikilizwa mbele ya watu.
    MTAJI
 msanii antakiwa awe na mtaji wa kutosha ili awe bora na aweze kuwalipa watu wake ,wacheza show wake,dj wake nk.
UBUNIFU,
msanii anatakiwa awe mbunifu wa kazi zake ,wengi watanzania wasanii hujtahidi sana kuwa wabunifu lakini kuna wengine sio wabunifu matokeo yake huiga kazi za wengine na hii haipendezi kwa mwanamziki
   msanii anatakiwa awe mbunifu kuanzia kwa jina lake mwenyewe,kazi zake,picha zake,blog yake,nk
 hii ni kwa wasanii wetu wa kitanzania jamani tuwashauri wasanii wetu

No comments: